Hatimaye beki wa kushoto wa Ruvu Shooting Edward Charles Manyama amevunjka ukimya na kueleza sarakasi za usajili wake kuelekea Azam FC, huku akiikacha Simba SC ambayo awali ilitangazwa imemsajili.

Manyama alichukua nafsi kubwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari mwezi Juni, kufuatisa usajili wake huko Azam Complex Chamazi kuleta taharuki miongoni mwa Mashabiki na Wanachama wa klabu ya Simba SC.

Saa 48 kabla ya kutambulishwa Azam FC, Mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari viliripoti alikua amesajiliwa na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, lakini baadae aliibukia Azam Complex Chamazi.

Manyama amesema: “Ni kweli nilifuatwa na Simba, lakini nilikubaliana na Azam FC baada ya kunipa dau nono, ndio maana sikutaka kuikataa ofa hiyo na hakuna mchezaji ambaye angekubali kuikataa ofa hiyo kwani soka ndio kazi inayotupa maisha,”

Manyama amesema uongozi wa Azam FC ulifuata taratibu za kumalizana na Ruvu Shooting, hivyo akaona kafanya uamuzi sahihi wa kuanza maisha mapya huko Azam Complex Chamazi kuanzia msimu ujao wa Ligi Kuu pamoja na Michuano ya Kimataifa.

“Nimeshakutana na viongozi wa timu zote kwa nyakati tofauti, ofa yangu ilikubaliwa na Azam FC ambao walifuata sheria zote kwenda kumalizana na Ruvu Shooting ambao walinipa baraka zote za kujiunga nao na msimu ujao nitavaa uzi wa Azam FC.”

Kabla ya kutua Ruvu Shooting wakati wa dirisha dogo la usajili mwishoni mwanzoni mwa mwaka huu na kusaini mkataba wa miezi sita, Manyama alikua mtumishi wa Namungo FC ambayo msimu huu iliiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika ‘CAF’.

Messi aiweka njia panda FC Barcelona
Mbeya wajipanga kubakiza timu zote Ligi Kuu