Kocha mkuu wa Young Africans Nasreddine Nabi amesema usajili mpya wa klabu hiyo kwa msimu ujao, utakuwa wa tofauti ukilinganisha na usajili uliofanywa mwanzoni mwa msimu huu.
Kocha Nabi ambaye alitua klabuni hapo kuchukua nafasi ya Kocha Cedric Kaze, amesema hatapokea mchezaji yoyote mpya ambaye ataletewa na kiongozi bila kujadiliwa na benchi la ufundi na kamati ya usajili.
Amesema kuna maskauti kutoka nchi mbalimbali za Afrika anajuana nao, atahakikisha anafanya nao kazi kwa ukaribu katika masuala ya ushauri na kupata wachezaji bora wa kigeni.
Hata hivyo kuna baadhi ya majina ya wachezaji wa ndani na nje yaliyofikishwa mezani kwa Kocha Nabi ili ayapitishe na.kisha wasajiliwe klabuni hapo, lakini ameyakataa kwa kigezo cha kukosa taratibu alizojiwekea.
Kocha Nabi amedhamiria kuwa na kikosi bora kwa msimu mpya wa Ligi Kuu na michuano ya kimataifa, kwa kukifanyia maboresho ya hali ya juu kikosi chake cha sasa.