Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imefanya marekebisho kwenye ratiba ya Ligi Kuu kwa kusogeza mbele siku moja tarehe ya kuchezwa michezo ya kumaliza msimu huu 2002-21.
TPLB imefanya mabadiliko hayo kufutia ombi la Uongozi wa Polisi Tanzania FC, baada ya kikosi chao kupata ajali ya gari siku ya Ijumaa (Julai 09) kilipokua kikitoka kwenye mazoezi mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Taarifa ya TPLB iliyosambazwa kwenye vyombo vya habari na kurasa za mitandao ya kijamii imeeleza kuwa, michezo ya mwisho ya Ligi Kuu iliyokua ichezwe Julai 14, sasa itachezwa Julai 15.
“Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kuhusu mabadiliko ya tarehe ya michezo ya mzunguko wa 33 wa Ligi Kuu ya Vodacom 2020/2021.”