”Sayansi ni sanaa na sanaa ni ubunifu”Hii ni kwa mujibu wa Tume ya sayansi na teknolojia Tanzania (COSTECH)
Tume hii yenye jukumu la kuishauri serikali kuhusu masuala yote yanayohusu sayansi teknolojia na ubunifu imesema inajivunia kuwa sehemu ya mafanikio muhimu ya wabunifu wa ndani wanaotumia vipaji vyao kutoa suluhuhisho ya changamoto mbalimbali zilizopo kwenye jamii.
Afisa uhusiano mwandamizi wa COSTECH Mary Kigosi amesema wamejipanga kuwaendeleza wabunifu wa ndani na kukuza taaluma ya uvumbuzi wa kisayansi kwa vijana mitaani na wale walio mashuleni.
Wakizungumza na Dar24media baadhi ya wabunifu na watafiti walio chini ya COSTECH wameishukuru tume hiyo kwa kuwawezesha kutimiza ndoto zao na kuahidi ubunifu zaidi kwa kazi za sanaa za kisayansi zitakazobadilisha jamii na kusaidia maendeleo ya nchi.
Kukua kwa teknolojia duniani kumetajwa kuchochewa kwa kiasi kikubwa kwa ongezeko la wabunifu wa kisayansi wanaogeza ujuzi wao kuwa faida kwa jamii.