*Serikali tumekuwa tukiendelea tukidhibiti ugonjwa wa Corona, kwani wapo majirani zetu wameshaingia waves ya nne.
*Maambukizi kweli yapo Kwenye baadhi ya Mikoa hivyo tunapaswa kuendelea kudhibiti,pia Vifo vipo , si kwa kiwango kikubwa Lakini hakuna haja ya kuwa na hofu kwani tutaendelea kuishi na COVID -19 na cha muhimu ni kupambana nao Kwa kunzigatia kinga .
*Serikali kuanzia awamu ya tano iliweza kuamsha Mambo mengi baada ya ugonjwa kutokea, na awamu hii ya sita inaendelea na Mhe. Rais ameweza kuunda kamati maalumu na walikuja na ushauri pamoja na mapendekezo 16 ambayo Karibu yote yametekelezwa .
*Mwaka jana Nchi iliweza kujiandaa kwa kuandaa miongozo na kutenga maeneo ambayo kama watu watapata maambukizi (isolation center).
Wizara tuliandaa miongozo 16 ya kudhibiti Corona ikiwemo ule wa elimu, upimaji, kudhibiti misongamano,uvaaji wa barakoa na mwitikio ulikua mkubwa ikiwepo barakoa za kushona wenyewe (barakoa za vitambaa)
Kunawa mikono pamoja na eneo la Tiba Asili na dawa za kisasa
*Nawasisitiza Wananchi kuendelea kujikinga na Corona kwa kuendelea kunawa mikono kwa maji Safi tiririka au vipukusi(Sanitazer), kufanya Mazoezi, kula lishe Bora na bila kusahau matumizi ya Tiba Asili.
*Wizara tuendelee kutoa elimu kwani upo upotoshaji mkubwa kwa Jamii kuhusiana na ugonjwa huu na njia za kukabiliana nao
*Kwenye mipaka tunao mkakati wa Kudhibiti kwa kupima abiria wote wanaoingia nchini lakini wananchi hawatakiwi kuwa na hofu kwa sababu sio Mara ya kwanza kupata milipuko duniani hivyo sisi tuendelee kuikabili.
*Pia Kwenye mikapa na viwanja vyetu vya ndege tumeweka wataalam wa kupima Corona , lazima tumpime mgeni yeyote anayewaili kwani Sasa hivi Kuna anuai mpya zinaibuka kila siku kutoka nchi nyingine hivyo inatusaidia kuzuia maambukizi ya anuani mpya.
*Watumishi waliosimamishwa kazi uwanja wa ndege wa JNIA walikosa nidhamu ya kazi Kwa kutokutii ratiba walizopangiwa, na hivyo kuathiri kazi za siku hiyo ikiwemo ndege zilizowasili na hivyo kuleta usumbufu. Kama kiongozi ukishamuonya kwa mdomo lazima na akarudia basi uchukua hatua nyingine lazima ichukuliwe
*Kama sekta ya afya tunaendelea kuhamasisha watu wajikinge Kwa sababu huu ugonjwa bado upo hata kama kuna chanjo duniani.
*Kinga mwili wako kwa kufanya mazoezi na kula Lishe Bora
*Lazima tuwakinge watu walio Kwenye kundi la kuathirika wakiwemo wenye kisukari,Moyo,uzito iliyopitiliza.
*Zoezi la kunawa mikono litasaidia watu wasipate maambukizi pia unawaji wa mikono unasaidia kuepusha Magonjwa mengine ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.
*Kuhusu chanjo sisi tumeshaomba na kuagiza chanjo hivyo tumeomba chanjo COVAX Facility za Aina mbalimbali ili kumpa Uhuru mwananchi kuchagua,zipo chanjo za Aina nne ,ndani ya miezi mitatu au minne tutakua tumeshapazipata na Serikali inafanya juhudi zingine za kuzipata mapema zaidi.
*Chanjo itaanza kutolewa kwa watu walio Kwenye hatari ya kuambukizwa Kama watumishi wa afya , wanaoenda kuhiji , wenye ulazima, na wanaosafiri Mara kwa mara na tumeshatoa muongozo wa kuratibu hizo chanjo.
Aidha tunamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jinsi anavyoshughulikia suala hili kwani na yeye ameamua Kupambana nalo hivyo tumuunge mkono na anaendeleza vyema Mikakati tuliyoanza nayo wakati wa awamu ya 5 na kuongeza Mikakati zaidi.
*Tumesema watu waepuke misongamano hivyo wanaoandaa shughuli zenye watu wengi na kusababisha misongamano mikubwa.. Professor amesisitiza “Nashauri kitalaamu Viongozi wa Kijamii, Wanasiasa na Wale wa Kidini Watafakari vyema kama kweli wanaulazima wa kufanya Mikusanyiko Mikubwa kwa wakati huu”
*Tunashauri Kwenye Mipira kusiwe na watu wengi ili kudhibiti maambukizi ,kuvaa barakoa na kunawa mikono kila mara.
*Wananchi wanayo nafasi ya kuhakikisha tunadhibiti huo ugonjwa Kama ilivyo mwaka jana kwani ugonjwa huu tutaendelea kuwa nao.
*Tunashauri Kwenye usafiri Ni vyema kuzingatia level seat na wananchi wavae barakoa
ALIYOSEMA MKURUGENZI WA MAENDELE YA BIASHARA, BW.WILSON MALOSHA
*Janga hili tumekuwa nalo kwa kipindi Sasa ,tutambue kuwa sekta ya biashara ni mtambuka,wizara ya afya imetupa muongozo wa Nini kifanyike ili shughuli ziweze kuendelea na wafanyabiashara wasiweze kupata maambukizi
*Tuendelee kufuata muongozo uliotolewa wa kujikinga na maambukizi kwa kuwana mikono kwa maji safi Safi tiririka na sabuni, vipukusi au social distance kwenye maduka madogo na makubwa,Malls, Bar, na Hoteli.
*Kila mmiliki niliowataja hapo juu ni vyema kuzingatia taratibu na msingi ambazo zimeanishwa Kwenye muongozo ili tuendelee na biashara kwani ndio msingi wa uchumi
*Kama nchi tunayo mahusiano ya nchi na nchi,kikanda na Kimataifa,hivyo tumekuwa na mikutano kwa njia ya mitandao ‘zoom’ hivyo wataalam wa Wizara,Taasisi za Umma na sekta binafsi wanaweza kujadili na kuweza kupata zile fursa mfano kuuza bidhaa Kwenye jumiya za ulaya hivyo kupitia njia hizo tumeweza kupata fursa hivyo biashara zimeweza kuimarika.
*mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade) na Shirika la Posta wameingia makubaliano ya kuanzisha e-shop ambayo ilizinduliwa mwaka huu Katika Maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF). Mfumo huu utatumika kuuza na kununua bidhaa kwa njia ya mtandao.
*Tukubali yapo maeneo na ngazi Fulani hatuwezi kufanya biashara kidigitali hivyo lazima wananchi waendelee kunawa mikono Mara kwa Mara wanapopokea fedha au kufanya huduma au kutumia sanitazer ili kuepuka na kuweza kuendelea na shughuli zao
*Tunavyo Vituo vya Huduma za Pamoja Mipakani (OSBP) ambavyo vinajumuisha Taasisi za Umma zinazoshughulikia biashara. Taasisi hizo ni TRA, TBS, WMA, UHAMIAJI, JESHI LA POLISI na TMDA na nyingineO ambazo kwa pamoja zina jukumu la kuhakikisha biashara mipakani inafanyika kwa kuzingatia miongozo ya Wizara ya Afya.
Imeandaliwa na Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto-Afya