Mshambuliaji wa Young Africans Waziri Junior Shentembo amekiri kuwa na huzuni, kufuatia kushindwa kufikia lengo alilojiwekea msimu huu 2020-21.
Waziri alisajiliwa Young Africans mwanzoni mwa msimu huu akitokea Mbao FC ya jijini Mwanza iliyoshuka daraja msimu uliopita.
Mshambuliaji huyo leo Jumatano (Julai 14), alizungumza na waandishi wa habari na kueleza namna anavyohuzunika kwa kushindwa kufikia lengo.
“Msimu huu mtu anayeongoza kwa ufungaji kwenye VPL ana magoli 15 msimu uliopita nilimaliza nikiwa na magoli 13 kwangu hiki kimeniuma lakini bado nitapambana ili nitimize lengo langu”. amesema Wazir Junior
Hata hivyo Waziri amekua na wakati mgumu wa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Young Africans tangu alipokuwepo Kocha Cedric Kaze.