Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango leo Julai 15, 2021 anatarajiwa kuanza ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma.

Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais anatarajia kuweka mawe ya msingi katika ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo kuweka jiwe la msingi katika ujenzi wa kituo cha kupoozea umeme eneo la Nguruka, jiwe la msingi ujenzi wa Chuo cha Ualimu Kabanga, jiwe la msingi ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Kasulu, jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Uvinza pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kakonko.

Aidha Makamu wa Rais atazindua Miradi mbalimbali ikiwemo ya Afya , Kufungua jengo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Mkoa wa Kigoma, kukagua maendeleo ya baadhi ya miradi katika mkoa huo pamoja na kuwasalimu wananchi katika maeneo mbalimbali atakayotembelea.

Dili la Haaland laota mbawa
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 15, 2021