Washika Bunduki wa Kaskazini mwa Jijini London, England klabu ya Arsenal inaangalia uwezekano wa kumsajili Mshambuliaji wa Mabingwa wa soka Ulaya Chelsea FC Tammy Abraham.
Arsenal wameweka nia hiyo katika kipindi hiki cha dirisha la usajili wakiamini watafanikisha mpango wa kumnasa Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23.
Chelsea FC imemuweka sokoni Tammy ili kupata kiasi cha pesa kinachoweza kukitumia kumsajili Mshambuliaji mmoja wa kati ya Harry Kane, 27, Romelu Lukaku, 28, au Erling Haaland katika dirisha hili.
Sababu kubwa ya Tammy kuwekwa sokoni ni kutokana na kutokuwa sehemu ya mipango ya meneja wa Mabingwa hao wa Ulaya Thomas Tuchel kwa msimu ujao kwani hata katika michezo ya mwisho ya msimu uliopita alikuwa hapewi nafasi ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza.
Kwa upande wa Araenal wamejitosa kwenye dili hilo, kufuatia Mshambuliaji wao kutoka Ufaransa Lacazatte kuwa mbioni kuondoka.
Mkataba wa Mshambuliaji huyo upo ukingoni na hakuna jitihada za kuuboresha zinazooneshwa na uongozi wa The Gunners.