Kocha Mkuu wa klabu ya Simba SC Didier Gomes ameishauri Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu hiyo kuwa kutokana na ligi ya Tanzania kuchelewa kuisha amewaomba baada ya fainali ya kombe la shirikisho (ASFC) dhidi ya Young Africans itakayochezwa Julai 25 Mkoani Kigoma, wachezaji wapewa mapumziko ya juma moja na August 01 warudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao (2021/22)

Gomes amedai kuwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champion League) itaanza mwanzoni mwa mwezi Septemba hivyo anataka kupata muda wa mwezi mzima kuandaa kikosi chake.

Pia ameutaka uongozi huo kutobadili sana kikosi kwa sababu wanaweza wakaanza upya na yasijirudie ya msimu wa 2019/20 ya kutolewa mapema.

Uongozi wa Bodi ya klabu ya Simba umebariki ratiba hiyo na kwa sasa unakamilisha usajili wa wachezaji 5 wapya ikiwa 3 wa ndani (ambao tayari) na 2 wa kimataifa (ambao wapo mbioni kukamilisha).

Wakati huo huo Uongozi umesema kambi ya maandalizi ya msimu ujao itakuwa nchini Misri na wameshapanga tayari na michezo ya kirafiki na timu kubwa za Misri kama Al Ahly.

Arsenal yajitosa kwa Tammy Abraham
Hadithi za 'MAGWIJI' zinafanana