Arsenal wamekubali mpango wa kumsajili beki wa kati wa Brighton, Ben White kwa ada inayodhaniwa kuwa karibu pauni milioni 50.

Kabla ya kuvunja benki kumnasa beki huyo kutoka England, Arsenal walikuwa na ofa ya pauni milioni 40 iliyokataliwa mnamo Juni na dau lingine kwa bei ya pauni milioni 47 baadaye pia ilikataliwa.

Lakini pamoja na majadiliano ya kina hadi Julai, vilabu hivyo vimeweza kufikia makubaliano, Bado kuna kazi ndogo ndogo za kufanywa kabla ya uhamisho kukamilika na mchezaji huyo wa miaka 23 anatarajiwa kufanyiwa vipimo atakaporudi kutoka likizo mnamo Julai 26.

Baada ya kuondoka Southampton mnamo 2014, White alipata uhamisho wa kwenda Brighton na mwishowe akatolewa kwa mkopo huko Newport County, Peterborough United na Leeds United.

Aliporejea na kuingia kikosi cha kwanza alikuwa bora msimu uliopita kwenye PL na alichaguliwa na Gareth Southgate kwenye kikosi cha England katika Fainali za Euro 2020.

Alisaidia pia Brighton kunusurika kushuka daraja na kumaliza nafasi ya 16 katika msimamo wa Premier League.

The Gunners wanataka kuimarisha safu yao ya ulinzi baada ya kumaliza nafasi ya nane kwenye Ligi na kukosa kucheza michuano ya vilabu barani Ulaya kwa mara ya kwanza tangu msimu wa 1994-95

Samatta kuvaa jezi namba 15
Arsenal yajitosa kwa Tammy Abraham