Mshambuliaji kutoka DR Congo na klabu ya Azam FC, Mpiana Mozinzi ataachana na klabu hiyo baada ya msimu huu 2020-21, utakaofiKia tamati kesho Jumapili (Julai 18).

Azam FC ilimsajili Monzinzi akitokea FC Lupopo ya mjini Kinshasa, DR Congo inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini humo.

Mshambuliaji huyo aliyetua nchini kwa mbwembwe wakati wa dirisha dogo mwanzoni mwaka huu, amefichua siri ya kuondoka kwake Azam Complex Chamazi.

Monzinzi amesema aliamini angeweza kumalizia mkataba wake lakini hata hivyo Azam FC imeamua tofauti na hana tatizo na uamuzi huo.

“Nimeambiwa na meneja wangu kwamba Azam FC ipo katika mazungumzo ya kusitisha mkataba wangu sina tatizo na hilo wakati wowote nitarejea nyumbani,” amesema Monzinzi.

Hata hivyo Mshambuliaji huyo tangu alipotua klabuni hapo amefanikiwa kufunga bao moja tu! Huku akishindwa kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha George Lwabdamina.

Mugalu: Msimu ujao nitafanya makubwa zaidi
Nabi: Naiheshimu sana Simba SC