Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi anatarajiwa kutua nchini wiki ijayo kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya kurejea kwa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Okwi atatua nchini akitokea kwao Uganda ambapo alirejea tangu mwezi uliopita baada ya kumaliza mkataba na klabu yake ya El Itihad ya Misri.
“Nimezungumza na Okwi na amenieleza anakuja nchini mapema wiki ijayo, naamini anarudi nyumbani,” kilisema kwa kifupi chanzo cha taatifa hizi.
Hata hivyo Okwi alishindwa kusema anakuja nchini kukamilisha mazungumzo au ameshamalizana na waajiri wake hao wa zamani.
“Ninasubiria tu muda,” Okwi amesema kwa kifupi.
Simba SC inatarajiwa kuanza makeke ya usajili baada ya kumaliza mchezo wa Fainali Kombe la Shirikisho dhidi Young Africans utakaochezwa kesho (Julai 25), Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma.