Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi amesema kuwa serikali inaboresha inaboresha huduma za upatikanaji wa vyeti vya chanjo ya corna kwa kukamilisha utaratibu wa kuhama kutoka kwenye mfumo wa vyeti vya makaratasi/vitabu na kwenda kwenye mfumo wa vyeti vya kidijitali.

Amesema hayo leo Augosti 8, 2021 wakati akitoa taarifa kuhusu maendeleo ya usambazaji na utoaji wa chanjo ya Covid-19 kwa wananchi unaoendelea nchi nzima.

“Naomba kuwakikishia wananchi kuwa taarifa zote za usajili na vyeti kwa wale waliochanjwa zimeandikwa katika vitabu na baadae taarifa hizo zitahamishiwa katika mfumo wa ki-elekroniki,” amesema.

“Ikumbukwe kuwa, wizara inafahamu mfuatano wa namba zake na zimetolewa kituo gani hivyo, ikitokea namba moja imejirudia uchunguzi utaanzia kwa watoa huduma waliotoa namba hizo na wateja wenye vyeti vya namba hizo.

Amesema kuwa kadi maalum za kieletroniki zinazoendelea kuandaliwa zitakuwa na vigezo vya kimataifa vya uthibitisho wa kupata chanjo ambapo vigezo hivyo ni pamoja na kuwa na utambulisho wa siri ambayo itajumuisha taarifa za mpokeaji chanjo, chanjo aliyopata, muda na mahali alipopata chanjo husika.

Profesa Makubi amesema Serikali inatoa tahadhari iwapo kuna watu watakao jaribu kujipatia vyeti vya chanjo kwa njia za udanganyifu, kuwa watabainiwa na mfumo na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Amesema kadi hizo zitatolewa kwa watu wote waliochanja hata wale ambao kwa sasa wamepewa cheti cha nakala ngumu nao watafikiwa ili kupewa cheti kipya ambacho kitasomeka kwenye mfumo wa kieletroniki.

“Natoa maelekezo kwa watoa huduma kuwa, pasiwepo na sababu yoyote ya walengwa wa uchanjaji kukosa au kukataliwa huduma; kama ni suala la vitambulisho, basi serikali za mitaa zisaidie kuwatambulisha walengwa hawa, hasa wazee,” amesema.

Itakumbukwa kuwa zoezi la uchanjaji Agosti 3, rekodi ya makundi ya walengwa peke yake kufikia Agosti 7 ilionyesha zaidi 164,500 walikuwa wameshajiandikisha (booking) kwa ajili ya kupatiwa chanjo wiki hii huku wengine 105,745 wakiwa tayari wamechanjwa.

Ametoa wito kwa wananchi katika yale makundi yaliyoainishwa kupata chanjo kuendelea kujitokeza ili kuweza kutumia huduma hiyo huku  vituo vyote vikiagizwa kuwa wazi hata siku za mwisho wa juma.

Ibenge ashinikiza usajili wa Mugalu
Wanaosadikiwa kuwa majambazi wauawa Lindi