Nahodha na Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Argentina Lionel Adres Messi amemwaga machozi wakati akitoa neno shukurani kwa viongozi, mashabiki na wachezaji wa FC Barcelona leo Jumapili (Agosti 08).

Messi amelazimika kuaga klabuni japo, kufuatia kushindwa kuafikiana na uongozi wa FC Barcelona suala la mkataba mpya.

Mshambuliaji huyo aliedumu Camp Nou kwa zaidi ya miongo miwili tangu akiwa kijana mdogo, ametoa maneno ya kusikitisha huku akikiri kuwa, alikua tayari kubaki FC Barcelona lakini mzingira ya kushindwa kuafikiana suala la mkataba mpya yanamuondoa klabuni hapo.

Messi amesema: “Nilishawishika kuendelea kusalia hapa Barcelona. Hapa ni nyumabni kwangu, na hapa ni nyumbani kwetu. Nilitaka kuendelea kubaki Barcelona na ilikuwa mpango wangu…lakini leo baada ya kuwa hapa kwa mda mrefu nalazimika kusema kwa kheri”

“Mkataba wangu mpya ulikuwa tayari umekamilika. Na nilipotoka mapumziko nilifahamu ningefika na kusaini tu, lakini dakika za mwisho naambiwa na rais Laporta, La Liga wamezuia dili hilo kukamilika”

“Habari zilizotoka Alhamisi za Barcelona na Laporta kusema kuwa waliniambia nipunguze mshahara wangu kwa 30% siyo kweli, ni uongo. Mimi ndio nilitoa Ofa ya kupunguziwa mshahara wangu kwa 50% lakini hamna kilichoendelea,”

“PSG wana nafasi ya kunisajili. Lakini mpaka sasa hakuna kilichokamilika, nilipokea simu nyingi baada ya Barcelona kuthibitisha kuwa naondoka, lakini mazungumzo yanaendelea.”

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 9, 2021
Djigui atambulishwa rasmi Young Africans