Waziri wa Kilimo Prof. Adolf Mkenda ameagiza kuondolewa kwa Kaimu Meneja wa Kitengo cha Ununuzi wa Mbolea kwa Pamoja (BPS) kilichopo katika Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) Nganga Nkonya na kuhamishiwa Wizarani kwa ajili ya kupangiwa majukumu mengine.

Amesema hayo wakati akizungumza na kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa mbolea uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

“Sisi mbolea ni suala la kufa na kupona sio suala la mzaha kama alivyokuwa anafanya, kulikuwa na mtu anajaribu kucheza na mfumo huo jambo lililopelekea kuchelewa kwa upatikanaji wa mbolea kwa wingi na kwa wakati” amesema Mkenda

Ameongeza kuwa serikali itaendelea kufanya mapitio ya mfumo huo kwa kutafuta namna nzuri ya kumsaidia mkulima kwa ajili ya upatikanaji wa mbolea.

Kuhusu bei ya mbolea kupanda, Waziri Mkenda amesema kuwa hilo ni tatizo la Dunia nzima kwani soko la Dunia limepanda kwa kiasi kikubwa ikiwemo gharama za usafirishaji.

Ameeleza kuwa Serikali imeielekeza Mamlaka ya Mbolea Tanzania (TFRA) kuanza kutoa vibali vya kuuza mbolea ambayo imeshaingia nchini (Export Permit) badala ya vibali hivyo kutolewa ofisi ya Waziri wa Kilimo.

Ili kuongeza ufanisi zaidi wa utendaji Waziri Mkenda amesema kuwa vibali hivyo vitatolewa kwa njia ya mtandao (Online) badala yake Ofisi ya Waziri wa Kilimo itakuwa na jukumu la kupewa taarifa ya utekelezaji wa utoaji vibali uliofanywa na TFRA.

Mahakama yaridhia kuongezwa
Jeshi la Rwanda lavunja ngome ya 'Al-Shabaab' Msumbiji