Wakili Peter Kibatala ambaye anamwakilisha mshitakiwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe katika kesi dhidi ya ugaidi, amewasilisha ombi la kuongeza kiapo cha ziada katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji John Mgeta.

Aidha Mahakama Kuu imeridhia maombi ya kuongeza kiapo cha ziada kwenye kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti huyo.

Wakili Kibatala pia ameomba Mahakama hiyo itoe samansi kwa mteja wake kuwepo mahakamani hapo shauri hilo litakapotajwa.

Hata hivyo upande wa Jamhuri wenye jopo la mawakili saba ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Hangi Changa umesema hauna pingamizi na maombi hayo hivyo kuomba mahakama kupanga tarehe nyingine kutajwa kwa shauri hilo.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Jaji Mgeta ameahirisha shauri hilo hadi Agosti 30, 2021 kwa ajili ya kutajwa.

Aliyesababisha ajali na kuua wanafunzi wawili atakiwa kujisalimisha
Waziri wa kilimo amtumbua Meneja ununuzi wa mbolea.