Mkuu wa Wilaya ya Mbeya ,Dkt. Rashid Chuachua amepiga marufuku magari ya matangazo ya misiba katika Jiji hilo baada ya kuchukua miili ya watu waliofariki kwenye hospitali za Serikali, huku akidai kuwa jambo hilo huleta taharuki kwa wananchi kitu ambacho hupelekea watu kuwa na hofu.

Aidh DC Chuachua ameagiza kamati ya ulinzi na usalama kufanya doria na kuwachukulia hatua wamiliki wa magari hayo watakaobainika.

“Kumekuwa na tabia ya familia za watu wanaopoteza maisha kukodi magari ya matangazo na kuanza kutangaza maeneo mbalimbali ya jiji na kutaja majina ya wapendwa wao sasa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa nimepiga marufuku rasmi leo Agosti, 10 2021,” Amesema DC Chuachua.

Hata hivyo DC Chuachua ameagiz zoezi hilo kuanza mara moja huku akitoa maelekezo kwa wanandugu wanaopata msiba kuwasiliana kama familia kufanya taratibu za mazishi lakini kuhusu suala la matangazo kutoka hospitali mpaka kwenye maziko marufuku,

Hali kadhalika amewahasa wananchi kuendelea kujikinga na ugonjwa wa Uviko 19 ikiwemo kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima, kunawa mikono kwa maji tiririka, kutumia vitakasa mikono lakini pia kuvaa barakoa.

Naye Mstahiki Meya wa jiji la Mbeya ,Dourmohamed Issa amempongeza DC kwa uamuzi huo sahihi ambapo amesema kuwa hatua hiyo aliyoichukua itasaidida kuondoa taharuki katika jamii.

Mabula asikitishwa wamiliki kutolipa gharama za upimajitoa
Ugonjwa wa marburg wazua gumzo Guinea