Wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya CECAFA KAGAME CUO, klabu ya Azam FC wametupwa nje ya michuano hiyo, baada ya kupoteza kwa changamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya timu mwalikwa kutoka Malawi Nyasa Big Bullets.

Dakika 120 za mchezo huo uliounguruma Uwanja wa Azam Complex Chamazi, zilishuhudia timu hizo zikitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.

Katika mikwaju ya penati Azam FC imepoteza kwa kufungwa 4-2, na sasa itakutana na KMKM kwenye mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.

Nyassa Big Bullets watacheza mchezo wa fainali dhidi ya Express ya Uganda iliyoitoa KMKM kwa mabao 2-1.

Gharama za upimaji Uviko 19 kwa wasafiri nchini zapungua
TFF yakutana na wawakilishi wa nchi