Mwanadada mmoja raia Korea Kusini An San (20) ametakiwa kurudisha medali tatu za dhahabu alizoshinda katika mashindano hayo ambayo yalifikia tamati wiki iliyopita.

An mwenye umri wa miaka 20, amepata umaarufu mkubwa kutokea Korea Kusini kutokana na kushinda medali tatu za dhahabu, ametakiwa kufanya hivyo na wanaharakati wanaopiga haki za wanawake nchini humo ‘anti feminists’ kutokana na staili yake ya kukata nywele ambayo wanaharakati hao wanasema sio staili ya kuwekwa na mwanamke.

Nchi ya Korea Kusini ni nchi ya 12 duniani kwa kuwa na uchumi mkubwa na kukua kwa teknolojia lakini ni nchi ambayo bado inakumbana na athari za mfumo dume ambao umeweka vigezo mbalimbali kwa wanawake ikiwemo kutonyoa nywele jambo ambalo linatafsiriwa kama tabia ya kiume.

Varane wa Simba SC kuondoka leo
Kambi ya Morocco kumnufaisha Matola kimasomo