Timu tatu kutoka Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na kati (CECAFA) Uganda, Tanzania na Sudan Kusini zitashiriki katika Michuano ya Wanawake ya COSAFA mwaka 2021 itakayofanyika kuanzia Septemba 15-26.

Timu nyingine zitakazoshiriki michuano hiyo ni mabingwa watetezi Afrika Kusini “Banyana Banyana” na Zambia ambao wametoka kushiriki michuano ya Olimpiki huko Tokyo.

Michuano hiyo itafanyika kwenye Uwanja wa Nelson Mandela Bay nchini Afrika Kusini.

Tanzania na Sudan Kusini zimepangwa Kundi B ambalo pia lina washindi wa pili wa mwaka 2020 Botswana na Zimbabwe.

Crested Cranes (Uganda) wamepangwa pamoja na Zambia, Namibia na Eswatini katika Kundi C.

Michuano hiyo itachezwa chini ya itifaki za COVID-19 kwa timu zote na maafisa wanaohusika na hakuna mashabiki watakaoruhusiwa katika viwanja.

Tanzania itakuwa inarejea kwa mwaka wa pili mfululizo ikiwa imecheza mnamo 2020 ambapo iliifunga Zimbabwe 1-0, lakini ikapoteza mbele ya Botswana katika hatua ya makundi na safari iliishia hapo hapo.

Kundi A: Afrika Kusini, Angola, Malawi, Msumbiji.

Kundi B: Botswana, Tanzania, Sudan Kusini, Zimbabwe.

Kundi C: Zambia, Namibia, Eswatini, Uganda.

Mwenyekiti wa kampuni za Asas afariki dunia
Rais Museveni awazawadia washindi wa Olimpiki