Mjumbe wa Bodi ya wakurungezi ya klabu ya Simba Zacharia Hanspope amesema kuwa klabu ya Simba iko mbali sana kwa sasa huwezi kuifanananisha na vilabu vya Tanzania kwenye usajili, kwenye uongozi na hata uendeshaji wa timu.
Hanspope amesema kuwa wanamatarajio ya kufanya vizuri kwani wamefanya maboresho ya wachezaji kwenye kikosi na wanatarajia wachezaji 3/4 wanaweza kuingia kwenye kikosi cha kwanza.
Pamoja na kuondoka baadhi ya wachezaji muhimu kwenye kikosi, Simba malengo yao kwenye ligi ya mabingwa Afrika msimu huu ni kufika robo fainali na kutetea ubingwa wa ligi kuu na kombe la shirikisho.
Mpaka sasa Hawa ndio wachezaji wa kigeni Simba SC mpaka sasa ni Joash Onyango (Kenya), Pascal Wawa (Ivory Coast), Thadeo Lwanga (Uganda), Bernard Morrison (Ghana) na Perfect Chikwende (Zimbabwe)
Wengine ni Rally Bwalya (Zambia), Meddie Kagere (Rwanda), Chris Mugalu (DR Congo), Peter Banda na Duncan Nyoni (Malawi).
Wanaoweza kuongezwa kwenye kikosi cha Simba ni Sadio Kanoute (Mali), Ousmane Sakho (Senegal) na Hennock Inonga (DR Congo)