Rais wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Wallace Karia, ameweka wazi kuwa sasa wachezaji wa kigeni watakaosajiliwa na timu watakuwa 12.

Karia amesema timu itaruhusiwa kutumia kwenye kikosi chake wachezaji 8 tu wa kigeni kucheza kwenye Michezo ya Ligi Kuu na madaraja ya chini kama timu zake zitafikisha idadi jiyo.

Kabla ya kiongozi hajathibitisha, tetesi za ongezeko la wachezaji wa kigeni kutoka wachezaji 10 hadi 12, zilichukua nafasi kubwa tangu mwanzoni mwa juma hili.

Hatua hiyo itaongeza chachu kwa klabu za Tanzania kufanya biashara ya kununua wachezaji kutoka nje ya nchi, ambao watawapa changamoto wachezaji wazawa ya kupambania nafasi kwenye vikosi vyao vya kwanza.

Pia maamuzi hayo ya mabadiliko ya usajili wa wachezaji wa kigeni, itaviimarisha vikosi vya klabu nne za Tanzania ambazo zitashiriki Michuano ya Kimataifa msimu wa 2021/22.

Simba SC na Young Africans zitashiriki Ligi ya Mabingwa Barani Afrika huku Azam FC na Biashara United zikishiriki Kombe la Shirikisho.

Pape Ousmane Sakho atambulishwa Simba SC
Azam FC yafafanua, Kwa nini imebadili nembo?