Uongozi wa Klabu ya Kagera Sugar umeendelea kutoa ufafanuzi wa sakata la Kiungo Mshambuliaji Yusuph Mhilu aliyetimkia Simba SC bila kufuata utaratibu.

Simba SC ilimtambulisha Mhilu juma lililopita kuwa sehemu ya kikosi chao kwa msimu wa 2021/22.

Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Ally Masoud amesema suala la Mhilu liko wazi, ni mchezaji wao halali.

Masoud amesema suala hilo lipo kisheria (Mkataba) na hawajakurupuka kuweka hadharani uhalali wa Mhilu na Kagera Sugar.

Ally Masoud amesema: “Mahusiano ya Yusuph Mhilu na Kagera Sugar ni mchezaji wetu halali kwa msimu mzima utakaoanza Septemba (2021), Yusuph Mhilu ni mchezaji halali wa Kagera Sugar”

“Yeye kusaini Simba na kutangazwa ndio madai (ya Kagera Sugar). Kwenye usajili lazima itatakiwa uambatanishe Release Letter (Barua ya kuachwa na Kagera), na kwenye system ya usajili lazima m-request (muombe) ili sisi tu-accept (tukubali)”

“Mpaka sasa tunavyoongea tuna shauri sisi na Mhilu linaloendelea TFF, tukiwa bado tupo ndani ya muda mpaka jumatatu ya wiki ijayo.”

“Yeye (Mhilu) ameomba, amepeleka shauri la kuomba tukae chini sisi na yeye kuvunja mkataba uliobaki na sisi”

“Kwa maana hiyo hata yeye Yusuph Mhilu anajua ana mkataba na Kagera Sugar”

Kuhusu kudai Milioni 200 ili kuvunja mkata wa Ally Masoud ameongeza: “Negociation ya kununua mkataba wa Mhilu ambayo inaendelea kati yetu na Simba bado ni siri na hatutaji figure (bei) kwenye vyombo vya habari wala mitandao ya kijamii”.

“Thamani ya Yusuph Mhilu ni kati yetu sisi, Simba na yeye mwenyewe mchezaji, tukifikia makubaliano kama tutaona ulazima upo tutataja ofa imeendaje na ada ya kuuzwa”

Boxer amtumia salamu Jesus Moloko
Hatma ya Cristiano Ronaldo Juventus njia panda