Aliyewahi kuwa Kocha Mkuu Lipuli FC na KMC FC Hererimana Haruna amejiunga na klabu ya Mbeya Kwanza FC, itakayoshiriki kwa mara ya kwanza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/22.
Kocha Hererimana amethibitishwa na Uongozi wa klabu hiyo kupitia kurasa za mitandao ya kijamii za klabu hiyo yenye maskani yake makuu jijini Mbeya, huku ikielezwa amesaini mkataba wa miaka miwili.
Klabla ya kutua klabuni hapo na kuthibitishwa rasmi, Klabu ya Mbeya Kwanza ilikua ikihusishwana mpango wa kumchukua kocha huyo, ambaye aliondoka nchini na kurudi kwao Burundi akitokea KMC FC.
Kocha aliyeipandisha daraja Mbeya Kwanza FC Steven Matata amekabidhiwa jukumu la kukinoa kikosi cha vijana cha klabu hiyo chini ya miaka 20, huku msaidizi wake Michael Hamis Mnyali akibakishwa kwenye benchi la ufundi kusaidiana na Kocha Hererimana.