Mabingwa wa Kihistoria katika Soka la Bongo Young Africans wamemtambulisha rasmi Beki kutoka DR Congo Yannick Bangala “Litombo”.

Young Africans wamethibisha kumnasa beki huyo wa zamani wa AS Vita Club, baada ya kuwasili mjini Markesh, Morocco usiku wa kuamkia leo Ijumaa (Agosti 20).

Bangala ana sifa ya kucheza zaidi ya nafasi moja uwanjani, ambapo nafasi nyingine anazozimudu ni beki wa pembeni na kiungo.

Usajili wa Beki huyo umeonheza idadi ya wachezaji kutoka DR Congo kwenye kikosi cha Young Africans cha msimu ujao wa 2021/22.

Wachezaji wengine kutoka DR Congo waliosajiliwa klabuni hapo ni Jesus Moloko, Heritier Makambo, Fiston Mayele na Mukoko Tonombe.

Sadio Kanoute atua Msimbazi
Azam FC yazindua jezi mpya