Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ameamuru wabunge wawili, Josephat Gwajima na Jerry Silaa kufika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ili kujibu tuhuma mbalimbali zinazowakabili ikiwemo kusema uongo na kushusha hadhi ya bunge.

Katika taarifa iliyotolewa leo Agosti 21, 2021 na Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa cha Bunge, Gwajima anatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Agosti 23, 2021 saa saba kamili mchana huku Silaa akitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Agosti 24, 2021 saa saba kamili mchana.

Endapo yoyote kati yao atashindwa kufika mbele ya kamati hizo kwa muda uliopangwa, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake kwa mujibu wa sheria ya kinga, haki na madaraka ya bunge.

Bashungwa azindua vifaa vya utafsiri lugha ya kiswahili BAKITA
Rais Samia awaapisha viongozi mbalimbali Ikulu Dar es Salaam