Kocha mkuu wa Young Africans Mohamed Nasreddine Nabi, amewaomba Mashabiki na Wanachama wa klabu hiyo kuacha kasumba ya kuwapa Presha wachezaji.

Kocha Nabi ambaye kwa sasa yupo safarini akitokea Morocco, amesema Wanachama na Mashabiki wanapaswa kuwapa muda wachezaji wa timu yao, na si kuwahimiza wafanye wanayoyataka kwa kipindi kifupi.

Amesema kuelekea msimu ujao anatarajia kuwa na timu imara na yenye ushindani, licha ya kupata muda mfupi wa kujiandaa kutokana na Ligi Kuu msimu uliopita kuchelewa kumalizika.

“Tuna wachezaji wapya wengi lakini ukiangalia ligi ilichelewa kuisha. Muda wa maandalizi umekuwa mchache, muda si mrefu wachezaji wataenda katika mataifa yao. Wakirudi tutakuwa na siku chache kabla ya kuanza Ligi ya Mabingwa Afrika (Caf Champion League) raundi ya awali. Mashabiki wasiongeze presha kwa wachezaji, wasubili ndani ya siku 90 wataona kitu.”

Young Africans imesitisha kambi ya nchinj Morocco, kufuatia wachezaji wao wanane kuitwa kwenye timu za taifa, kwa ajili ya michezo ya kufuzu fainali za Kombe la dunia 2022.

Ajali yauwa wafanyakazi watano wa TRA
Young Africans yasitisha kambi Morocco