Wafanyakazi watano wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) wamefariki dunia kwa ajali ya gari aina ya Land Cruiser lililogonga kwa nyuma Lori aina Fuso.
Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23, 2021 saa 11 alfajiri katika eneo la Hanseketwa wilayani Mbozi, Songwe.
Kamanda wa Polisi Janethi magomi amethibitisha kutokea kwaajali hiyo ambapo amelitaja gari ambalo limepata ajali ni aina ya Land Cruiser ambalo liligonga gari aina ya Fuso na kisha kuacha njia na kupindika.
Hata hivyo watumishi hao wa TRA ni kikosi kazi cha Fast Track ambao walikuwa wakilifukuza gari iliyodhaniwa kubeba bishaa za magendo.