Shirikisho la Soka Afrika “CAF” chini ya rais wake, Patrice Motsepe wameiomba Serikali ya Uingereza kuwaruhusu wachezaji wa Kiafrika kusafiri na kushiriki michezo ya kimataifa kwa nchi zao kuelekea mechi za kufuzu Kombe la Dunia mwezi ujao.

Taarifa ya CAF inakuja baada ya Klabu za Premier League kuamua kwa kauli moja kutowaachilia wachezaji kwa mechi za kimataifa katika mataifa yaliyo kwenye orodha nyekundu dhidi ya Uingereza mwezi ujao sababu ya janga la COVID-19.

Uamuzi huo umechukuliwa ili kuepusha wachezaji kulazimika kujitenga karantini kwa siku 10 ikiwa tu watarudi England….Taarifa iliyotolewa Jumanne ilisema:

“Klabu za Premier League leo kwa kauli moja wameamua kutowaachilia wachezaji kwa mechi za kimataifa zitazochezwa katika nchi zenye orodha nyekundu mwezi ujao.

“Uamuzi wa vilabu, ambao unaungwa mkono sana na Premier League, utatumika kwa wachezaji karibu 60 kutoka vilabu 19 vya Premier league ambao wanapaswa kusafiri kwenda nchi 26 zilizo na orodha nyekundu kwenye dirisha la kimataifa la mwezi Septemba”.

Argentina, Brazil na Misri ni miongoni mwa mataifa ambayo wananchi wake kwa sasa wako kwenye orodha nyekundu ya Serikali ya Uingereza kuhusu kusafiri kwenda Uingereza.

Brazil inaikaribisha Argentina kwenye Mashindano ya kufuzu Kombe la Dunia huko Maracana mnamo Septemba 5, lakini uamuzi wa PL unamaanisha wachezaji wengi watakosa mechi hiyo, na michezo mingine kadhaa mikubwa huko Amerika Kusini kama ilivyo kwa Misri kukatiliwa na Liverpool kumtumia Mohamed Salah huko Cairo dhidi ya Angola mnamo Septemba 2.

Kaduguda: Simba itayumba akiondoka Mohamed Dewji
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Augusti 26, 2021