Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC leo Alhamis (Agosti 26) watacheza mchezo wa pili wa Kirafiki wa Kimataifa wakiwa nchini Morocco.
Kikosi cha Simba SC chini ya Kocha Didier Gomes kitacheza dhidi ya Olympique Club de Khouribga ya Morocco.
Jana Jumatano (Agosti 25) kikosi cha Mabingwa hao kilifanya maandalizi ya mwisho tayari kwa mchezo huo wa kirafiki ambao ni sehemu ya Program ya kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hata hivyo katika mchezo wa leo, Simba SC itawakosa baadhi ya wachezaji wake walioitwa kwenye timu zao za taifa kwa ajili ya michezo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2022.
Mwishoni mwa juma lililopita Simba SC ilicheza mchezo wake wa kwanza wa Kimataifa wa Kirafiki dhidi ya FAR Rabat inayonolewa na Kocha Sven Vanderbrieck, na kupata sare ya mabao 2-2.
Mabao ya Simba SC katika nchezo huo yalifungwa na viungo Hassan Dilunga na Pappe Ousman Sakho.