Hatimaye Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC wamemalizana na Kagera Sugar, kuhusu
uhamisho wa Kiungo Mshambuliaji Yusuph Mhilu.
Klabu hizo ziliingia kwenye mzozo baada ya Simba SC kumtambulisha hadharani Mhilu kama mchezaji huru mwanzoni mwa mwezi Agosti.
Kagera Sugar walidai bado wana mkataba wa mwaka mmoja ya mchezaji huyo, hivyo walitishia kuweka pingamizi TFF, na ndipo Simba SC walipoomba suluhu ya mazungumzo.
Taarifa zilizotolewa na Kagera Sugar zimeeleza kuwa, Mhilu ameuzwa Simba SC kwa dau la Shilingi Milioni 40.
Hivyo uhamisho huu wa Mhilu kwenda Simba SC ni uhamisho ambao umehusisha kuvunja Mkataba wake wa Mwaka mmoja uliokuwa umesalia ndani ya Klabu ya Kagera Sugar.