Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Luteni Josephine Mwambashi, amefurahishwa na Wakala wa maji vijijini RUWASA kwa kutekeleza mradi mkubwa wa maji safi na salama wenye thamani ya shillingi Bilioni 163 katika Kijiji Cha Mkowela kata ya Namakambale Wilaya ya Tunduru mkoaani Ruvuma.

Akizindua mradi huo wa maji Mkowela Luteni Josephine Amesema kuwa mradi unakwenda kumaliza kabisa kero ya muda mrefu  ya maji safi na salama kwa wakazi wa kijiji cha Mkowela na kuharakisha maendeleo ya wakazi hao ambao  awali walilazimika kutumia maji yasio safi na salama kwa matumizi ya binadamu yaliyopatikana kwenye mito na  visima vya asili.

Aidha amewataka wataalam wa RUWASA, kuhakikisha wanatembelea mara kwa mara miradi ya maji inayotekelezwa ili kufahamu kama miradi hiyo inafanya kazi na pale inapoharibika waweze kufanya matengenezo ya haraka ili wananchi wasikose huduma ya maji katika maeneo.

Kwa upande wake,Mhandisi wa maji wa Ruwasa wilayani Tunduru Emmanuel Mfyoyi amesema,mradi huo uliibuliwa na wananchi kutokana na changamoto kubwa ya  upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ambapo Serikali kupitia wizara ya maji ilitoa fedha ili zisaidie  upatikanaji wa huduma ya maji kwa wananchi wa kijiji hicho, huku lengo likiwa  ni kuboresha huduma ya maji kwa wananchi chini ya kauli Mbiu  ya kumtua Mama ndoo kichwani kwa kusogeza huduma ya maji karibu na wananchi.

Sambamba na hayo yote kupitia Mwenge wa Uhuru Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigadia Jenerali Wibert Ibuge,amewataka Watanzania kutambua kuwa,falsafa ya Mwenge wa Uhuru imejikita katika kudumisha Amani,upendo,utulivu na mshikamano ili kujenga Taifa lenye maendeleo.

Wabunge wajengewa uelewa kuhusu Uviko 19
Wahandisi wahimizwa kujisajili