Kikosi cha wawakilishi wa Tanzania Bara kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Azam FC kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo asubuhi kuelekea mchezo wao wa mkondo wa pili dhidi ya Horseed FC ya Somalia.

Mchezo huo utachezwa kesho Jumamosi Uwanja wa Azam Complex saa 10:00 jioni, huku Azam FC wakiongoza kwa mabao 3-1, waliyoyapata kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa uwanjani hapo.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilino ya Azam FC Thabit Zakaria ‘ZAKA ZAKAZI’ amesema mipango yote ya maandalizi imekwenda vizuri, na wana matarajio makubwa ya kuendeleza wimbi la ushindi kama walivyofanya juma lililopita.

“Dhamira yetu ni kuendeleza ushindi kama tulivyofanya kwenye mchezo uliopita, tunajua haitokua rahisi, lakini tumejizatiti kufikia lengo hilo.”

Katika mchezo huo Azam FC watakua ugenini licha ya kucheza kwenye uwanja wao wa Azam Complex Chamazi, kufutia klabu ya Horseed kuomba mchezo wao wa mkondo wa pili kuchezwa jijini Dar es salaam, kufutia hali ya kiusalama nchini kwao Somalia.

Nyundo yawashukia makatibu tawala wa mikoa
Gomez kutumia mfumo mpya 2021/22