Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi amekipongeza kikosi cha Biashara United kwa kuwabana Simba SC kwenye mchezo wa mzunguuko wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2021/22.
Hapi ambaye alikua sehemu ya Mashabiki walioshuhudia mpambano huo uliopigwa Uwanja wa Karume mjini Musoma na kumalizika kwa sare ya 0-0, ametoa pongezi hizo sambamba na zawadi ya shulingi milioni 10.
“Nawapongeza vijana nawakabidhi milioni 10. Kuhusu penati imeleta maswali mengi sana,”
“Kazi imeisha. Tumeandika rekodi ya Biashara Utd kukataa kufungwa na Simba leo. Ni rekodi mpya chini ya awamu mpya ya Rais Samia na RC mpya. Na huyu ndiye golikipa aliyechomoa penati ya mbeleko. Dau lipo.” amesema Ally Hapi, Mkuu wa Mkoa wa Mara
Katika mchezo huo Simba SC ilipata penati dakika za lala salama, lakini Nahodha na Mshambuliaji John Bocco alishindwa kukwamisha mpira wavuni, baada ya mlinda mlango wa Biashara Utd kupagua shuti na mkongwe huyo.