Meneja wa Klabu Bingwa nchini England Manchester City, Pep Guardiola, amemwagia sifa za kutosha Malinda Lango wa PSG Gianluigi Donnaruma, kufuatia kiwango maridhawa alichokionesha kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya usiku wa kuamkia Jumatano (Septemba 28).

Katika mchezo huo Manchester City ilikubali kibano cha mabao 2-0 yaliyofungwa na Kiungo kutoka nchini Senegal Idrissa Gana Gueye pamoja na Mshambuliaji kutoka Argentina Lionel Messi.

Guardiola amesema kupoteza kwao, mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa mbele ya PSG ni moja ya vipindi, ambavyo vinatokea kwenye soka , hivyo wanakwenda kula vizuri na kupumzika, kwa ajili ya mchezo wao ujao, dhidi ya Liverpool kwenye Ligi Kuu England.

Guardiola amesema walicheza kwa mbinu za kusaka ushindi, lakini kilichotokea ni uimara wa kipa wa PSG, Donnaruma ambaye alifanya kazi kubwa kwenye kuokoa hatari za wachezaji wake.

“Tulikuwa tunahitaji ushindi na tumecheza namna hiyo, lakini ni sehemu ya matokeo na huwa inatokea kwenye soka. Yote kwa yote kipa wa PSG Donnaruma alifanya kazi yake kwa kuokoa hatari nyingi.

“Kwa matokeo, ambayo yametokea hamna namna tunakwenda kupumzika vizuri, kutafuta chakula na kula vizuri pamoja na kupata muda wa kumpumzika, kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wetu, dhidi ya Liverpool,” amesema.

Jumapili (Oktoba 03), Man City inayoshika nafasi ya pili, kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England ikiwa na alama 13, itakutana na Liverpool, ambayo ni vinara wakiwa na alama 14, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Anfield.

Ronald Koeman akata tamaa FC Barcelona
Nuno ajificha kwa wachezaji wake