Mahakama ya hakimu mkazi jijini Arusha imesogeza mbele tarehe ya hukumu ya kesi ya aliyekua Mkuu wa wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili iliyokua itolewe leo hadi oktoba 15, 2021.
Sabaya na wenzake wanakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha ambapo February 9, 2021 wakidaiwa kuvamia na kupora katika Duka la Saad Store linalomilikiwa na Mohamed Saad
Hukumu hiyo leo ilitakiwa kutolewa na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Odora Amworo.
Kesi ya Sabaya imekua ikisikilizwa kwa muda wa miezi miwili sasa tangu akamatwe na kutiwa hatiani na jeshi la polisi.