Wazee nchini leo wanaungana na wenzao wa mataifa mbalimbali kusherehekea siku ya Kimataifa ya Wazee inayoadhimishwa Oktoba Mosi ya kila mwaka, ikiwa na kauli mbiu ya Matumizi Sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa Rika Zote.
Katika kuadhimisha siku hiyo, Wazee katika maeneo mbalimbali wamekuwa wakikutana na kujadili mambo yanayowahusu.
Aidha Wazee wa Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya wameiomba Serikali kuwaboreshea huduma za afya kwa kuwa katika baadhi ya maeneo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kadhaa.
Kwa mujibu wa Baraza la Wazee wilayani Rungwe, zaidi ya Wazee elfu 24 wametambuliwa wilayani humo huku wakikabiliwa na changamoto kadhaa ikiwa ni pamoja kutopata huduma stahiki za afya.
Taasisi mbalimbali zinazoshughulikia masuala ya Wazee nazo hutumia siku ya Kimataifa ya Wazee kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili Wazee na kuzitafutia ufumbuzi.