Meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti ameponda kiwango cha kikosi chake, baada ya mchezo wa Ligi Kuu ya Hispania dhidi ya Espanyol walioibuka na ushindi wa mabao 2-0, mwishoni mwa juma lililopita.

Kichapo hicho kilikua cha pili mfululizo kwa Real Madrid ambao walitangulia kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Sheriff ya nchini Moldavia, katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Carlo Anceloti amesema mchezo dhidi ya Espanyol ulikua wa hovyo, na wachezaji wake walionyesha kiwango kibovu tangu alipoamua kurejea klabuni hapo kwa mara ya pili.

“Ulikuwa mchezo mbovu zaidi kwa msimu huu hadi sasa.”

“Tulicheza vibaya, hakuna cha kusema zaidi. Tunatakiwa kubadilisha mtazamo na akili yetu, ilikuwa ni wiki mbaya sana kwetu.”

“Kufungwa huku halikuwa tukio la bahati mbaya kwani tulistahili kupoteza mchezo. Tunahofu kwa sababu tumepoteza michezo miwili mfululizo na huu si utamaduni wa klabu hii, tunatakiwa kurekebisha makosa yetu.” amesema Anceloti.

Hata hivyo bado Real Madrid wanaendelea kuongoza msimamo wa ligi ya Hispania kwa kufikisha alama 17 sawa na wapinzani wao wa jijini Madrid (Atletico Madrid), lakini wametofautishwa na mabao ya kufunga na kufungwa.

Upande wa Ligi ya Mabingwa, Real Madrid inashika nafasi ya pili katikamsimamo wa kundi D kwa kufikisha alama 3, huku Sheriff ikiongoza msimamo wa kundi hilo kwa kufikisha alama 6.

Gerard Pique: Kuna tatizo kubwa Barca
Chelsea yamshangaza Antonio Conte