Timu ya KMC FC leo imeanza maandalizi yake kuelekea katika mchezo wa mzunguko wa tatu wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2021/2022 ambapo Oktoba 19 itakutana na Yanga katika uwanja wa Majimaji Songea.
KMC FC imeanza maandalizi hayo leo ikiwa ni baada ya kutoka katika michezo miwili ya ugenini ambayo ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania na Coast Union ya Mkoani Tanga ambapo kikosi hicho kilirejea jijini Dar es Salaam Oktoba tatu na kupewa mapumziko ya siku mbili kabla ya kuanza mazoezi hayo leo.
Michezo mingine ambayo itapigwa mwezi Oktoba ni pamoja na dhidi ya Namungo ambao utachezwa katika Uwanja wa Ilulu Oktoba 23, na mwingine ni dhidi ya Kagera Sugar ambao utapigwa Oktoba 29 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa.
Timu hi ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu John Simkoko na wasaidizi wake Habibu Kondo pamojana na Hamadi Ally wanaendelea kufanya maandalizi hayo ili kuhakikisha kwamba katika mchezo huo Timu inapata matokeo mazuri.
Aidha katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kwa muda kupisha Timu ya Taifa, kutakuwa na program mbalimbali ambazo makocha wameziandaa kwa ajili ya kuwaweka vizuri wachezaji na kwamba baada ya Ligi kurejea Timu iwezekufanya vizuri katika michezo hiyo.
Licha ya kutokuwa na matokeo mazuri katika michezo ya mwanzo wa msimu wa 2021/2022, lakini mikakati ya klabu ni kuhakikisha kwamba pamoja na ushindani uliopo katika msimu huu lakini itahakikisha inafanya vizuri katika michezo hiyo na mingine iliyopo kwenye ratiba ya ligi kuu.
Imetolewa leo Oktoba 6
Na Christina Mwagala
Afisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya KMC FC