Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amos Makalla Leo tarehe 07 Oktoba, 2021 amewataka TARURA kurekebisha Mfumo wa ada ya maegesho ambao umebadilika kwa sasa kutoka Analojia kwenda Digitali na kuleta adha mbalimbali kwa wananchi.
Makala amesema TARURA wanapaswa Mfumo wao usomane na wale wanaofanya nao kazi ili kuleta Matokeo Chanya kwa wananchi na sio kutembea peke yao.
Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa amewataka TARURA kuhakikisha “Control Number” ya kulipia inapatikana kwa Wakati.
Aidha, RC Makalla amewataka TARURA kutoa Elimu kwa Umma kuhusu Mfumo huo kwani wananchi wengi hawana uelewa na Mfumo huo.
Kwa upande wake Meneja wa TARURA Mkoa wa Dar es Salaam Mhandisi Geoffrey P. Mkinga amesema kuwa amepokea Maelekezo yote ya Mkuu wa Mkoa na kuahidi kuyafanyia kazi ili kuboresha utaratibu wa Ukusanyaji wa Mapato
“Maegesho ya Magari sio bure yanalipiwa ambapo kwa saa ni shilingi 500 na kwa siku nzima ni shilingi 4500”. Alisisitiza Mhandisi Geofrey P. Mkinga
miezi kadhaa iliyopita TARURA walianzisha mfumo mpya wa kulipia maegesho ya magari mjini ambapo mmiliki atatakiwa kulipa ada hiyo kwa kutumia namba ya malipo atakoandikiwa kwa kutumia namba ya gari na sio kutoa mkononi kwa watu wanaokatisha ushuru.