Halmashauri ya MAFINGA wanaendelea na uhamasishaji wa chanjo DHIDI ya UVIKO-19 kwa Wananchi wa Wilaya hiyo.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji MAFINGA Dkt.Innocent Mhagama amesema kuwa Halmashauri hiyo imejipanga Katika kutoa elimu kwa wananchi ikiwemo Kwenye shughuli zao za Kila siku.

“Kama Halmashauri tunaendelea kuhamasisha Kwenye Mitaa yetu ikiwemo maeneyo ya makazi,mtaa kwa mtaa ili kuhakikisha wananchi wanaelewa.

Aidha, Dkt Mhagama amesema Katika kutekeleza Mpango wa Jamii Shirikishi na Harakishi na Harakishi wa uhamasishaji dhidi ya chanjo ya UVIKO-19 wameweza kukutana na wafanyabiashara wote wa Mji na wameweza kuwapatia elimu na kuwajibu maswali yaliyokuwa yakiwatatuza hapo awali.

Ameongeza kuwa wananchi wengi walikua na maswali ambayo walikua na taarifa potofu kuhusu Chanjo hizo na ziliwafanya wasiweze kuchanja Ila kwa elimu waliyowapatia wameelewa na wamehamasika kuchanja.

Dkt.Mhagama amekiri kwamba awali muitukio ulikua ni Mdogo Ila baada ya kutoa elimu kila mahali wananchi wameweza kujitokeza na kuchanja kwa wingi.

Gadiel: Muda wangu ukifika nitacheza
Rais Samia afanya uteuzi