Dakika chache baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumhukumu miaka 30 jela aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili, ikiwatia hatiani kwa makosa ya unyang’anyi wa kutumia silaha, amewatumia ujumbe watanzania.
Sabaya ametaka Watanzania ambao amewaita ‘ndugu zake’ kutoogopa kwakuwa Mwenyezi Mungu yuko kazini.
“Ndugu zangu msiogope Mungu yupo kazini,” alisema Sabaya.
Hakimu Omworo amesema kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha. Hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.
Sabaya na wenzake walifikishwa mahakamani leo saa 3:05 asubuhi, kwa ajili ya hukumu ambayo imekamilika baada ya kusikilizwa kwa kipindi cha miezi sita.