kurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) amewafutia mashitaka 10 ya utakatishaji fedha washtakiwa watatu kati ya watano akiwemo aliyekuwa Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu.

Awali washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashitaka 55 likiwamo utakatishaji fedha na kuisababishia Serikali hasara ya Sh1.175 bilioni.

Washitakiwa wengine waliofutiwa mashitaka hayo ni aliyekuwa Ofisa Usafirishaji Nida, George Ntalima na Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ladslaus Komanya kesi hiyo iko katika hatua za usikilizwaji lakini Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) amekusudia kufanya marekebisho madogo chini ya kifungu cha 234(1) cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai (CPA).

“Jumla ya mashtaka yaliyokuwa yanawakabili ni 55, baada ya marekebisho haya yatakuwa mashtaka 45, kwa mshtakiwa wa kwanza Dickson Maimu, mshtakiwa wa tatu, George Ntalima na wa nne Xavery Silverius maarufu Silverius Kayombo ambao wameondolewa mashtaka ya utakatishaji fedha,” amedai Wakili Komanya.

“Hata mkiwasilisha hati mpya, kesi hii haiko haiko mbele yangu, nawashauri muiwasilishe mbele ya Hakimu husika tarehe itakayopangwa, na kuhusu dhamana nawashauri kuwasilisha maombi Mahakama Kuu,” amesema Hakimu Shaidi.

Baada ya maelezo hayo kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 4 itakapotajwa ambapo upande wa mashtaka utawasilisha hati mpya.

Rais Samia atoa maagizo kwa uongozi UWT
Biteko arahisisha biashara ya madini Ulanga