Tafiti za kisayansi zinaonyesha kuwa Mlima Kilimanjaro, uliopo nchini Tanzania umepoteza asilimia 90 ya barafu yake katika kipindi cha miaka 100 iliyopita.

Wanasayansi hao akiwemo Profesa Clavery Tungaraza wa Tanzania na Dk Doug Hardy kutoka Marekani ambaye alikuwa miongoni mwa wanasayansi wa kwanza kabisa kufanya utafiti mlima Kilimanjaro, wamesema kama hatua hazitachukuliwa huenda barafu ikatoweka kabisa katika kipindi cha miaka michache ijayo.

Simon Mtuy amepanda mlima Kilimanjaro mara nyingi na familia yake imekuwa ikilima katika miteremko ya mlima huo kwa karnekadhaa sasa, amesema kuwa katika maisha yake ameshuhudia mabadiliko makubwa katika mlima huo na hali ya hewa.

Mlima huo mrefu kuliko yote Afrika, ukiwa na mita 5,895 ni mmoja kati ya milima mirefu Afrika Mashariki inayopoteza barafu.

Mwendesha Mashtaka Sudan afutwa kazi
Biashara United Mara yasaini dili la mamilioni