Jumla ya wahamiaji haramu 1,152 wamekamatwa na Idara ya Uhamiaji mkoani Kagera, katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia Agosti hadi Oktoba mwaka huu, baada ya kubainika kuingia kinyemela katika maeneo mbalimbali mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Uhamiaji mkoa wa Kagera Thomas Fussy, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameelezea ni kwa namna gani hiyo inakabiliana na tatizo la watu wasio raia kuingia hapa nchini bila kufuata utaratibu.
Fussy amesema kuwa wahamiaji 1,133 wamerejeshwa nchini mwao na wengine tisa wamefikishwa mahakamani.
Ameeleza kuwa wamefikia uamuzi wa kurejesha idadi kubwa ya wahamaji hao nchini mwao ili kuepusha kuongeza msongamano katika magereza, kutokana na uwepo wa ugonjwa wa COVID-19.