Kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaotuhumiwa kwa makosa ya ugaidi inaendelea kusikilizwa leo Novemba 4, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.
Mahakama hiyo leo inatarajiwa kuendelea kupokea ushahidi wa upande wa mashtaka kutoka kwa shahidi wa sita.
Itakumbukwa kuwa kesi hiyo ilishindwa kuendelea jana baada ya shahidi aliyekuwa ameandaliwa kushindwa kufika mahakamani kutokana na kuugua.
Tayari washtakiwa wameshafikishwa kwenye chumba cha mahakama na Mawakili wa pande zote pia wameshafika mahakamani mpaka sasa ni Jaji Joachim Tiganga ndiye anayesubiriwa.