Kocha Mkuu wa Young Africans Nesreddine Mohamed Nabi alikua miongoni mwa watazamaji wa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba SC dhidi ya Namungo FC, uliochezwa jana Jumatano (Novemba 02), Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Kocha huyo ambaye ameiongoza Young Africans kuibuka na ushindi kwenye mchezo mitano mfululizo ya Ligi Kuu Bara, alionekana kuwa mtulivu huku akiwa ameshika tama ishara ya kuufuatilia mchezo huo kwa umakini mkubwa.

Nabi alikuwa amevalia kofia nyeusi, alionekana kuwasoma Namungo FC ambao baada ya wiki ya Kimataifa atakuwa na mchezo dhidi yao Novemba 20, Uwanja wa Ilulu mkoani Lindi.

Hiyo ilikua fursa kwa kocha huyo kutoka nchini Tunisia kuona namna gani mbavyo atawaandaa vijana wake kwa ajili ya mchezo huo.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya Young Africans kucheza dhidi ya Namungo watarejea jijini Dar es Salaam kucheza dhidi ya Mbeya Kwanza kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Desemba 12.

Kocha Nabi hakuwa pekee yake uwanjani hapa, alikuwa na kocha msaidizi Cedric Kaze, meneja wa Young Africans, Hafidh Saleh licha ya kuwa walikaa sehemu mbili tofauti mmoja, VIP A na mwingine B.

Chama atamani kurudi Simba SC
Matola: Tutapata ufumbuzi wa tatizo letu