Takribani miezi miwili pekee imesalia kuelekea kuumaliza mwaka 2021, ambapo mara nyingi utaratibu wa wasanii wengi kote duniani katika kipindi kama hiki huandaa matamasha maalum ya funga mwaka ambayo kwa hapa nyumbani Tanzania wasanii wengi wamekuwa wakichagua kurejea katika maeneo waliyotokea kwaajili ya kwenda kusambaza burudani ya shukurani kwa kuandaa matamasha, hafla za kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji, wanafunzi mashulenink.

Kutoka Konde music worldwide Lebal ya muziki iliyo chini ya msanii Harmonize, Hatimaye wamerejea na taarifa ya ujio wa tamasha la kwanza maalumu kwa ajili ya msanii wao wa kwanza kusainiwa chini ya Lebal hiyo maarufu nchini, tamasha maalumu la funga mwaka litakalo fanyika mkoani mtwara Nov 27, mwaka huu 2021.

Ibraah ameweka wazi mapokezi ya taarifa za mpango huo ulioandaliwa na uongozi wake kuhusu kurudi kutoa shukrani kwa kuwaburudisha wananchi wa mkoa wa Mtwara ikiwa ni sehemu ya shukurani kwa kuendelea kumuunga mkono katika mapambano ya kupeleka mbali muziki wake.

“Ni takribani mwaka mmoja sasa toka nimeanza kufahamika kwenye kiwanda hiki cha muziki wa Kizazi kipya na ndoto yangu kubwa ilikua siku moja niweze kufanya show kubwa nyumbani sehemu ambayo imenilea na kunikuza MTWARA…hatimaye Historia inaenda kuandikwa pale nangwanda Sijaona Mtwara, narudi nyumbani Tafadhari Naomba Mnipokee” alisema Ibraah.

Ibraah kwa sasa ni mmoja wa wasanii Chipukizi wenye kufanya vizuri kwenye kiwanda cha muziki Afrika Mashariki akiwa na Extended Playlist (EP) yenye nyimbo takribani 6, alizoshirikiana na wasanii mbali mbali kutoka mataifa kadhaa barani Afrika, ikiwa ni pamoja na nyimbo kadhaa zinazoendelea kufanya vizuri kwenye chati mbali mbali za muziki Afrika.

RC Makalla ataja mambo ya kuzingatiwa baada ya kuwapanga Machinga Dar.
Chama atamani kurudi Simba SC