Baada ya kutiwa mbaroni kwa takribani wiki moja hatimaye rapa Fetty Wap ameachiwa huru kutoka Jela kwa dhamani ya USD 500k ambazo ni sawa zaidi ya 1.1 Bilioni kwa pesa za Kitanzania.
Rapa huyo maarufu alikamatwa na Polisi akiwa na wenzake watano wakiwa katika tamasha la Rolling Loud, mapema wiki iliyopita kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya uuzaji na usambazaji wa Dawa za kulevya.
“Kama inavyodaiwa, washtakiwa walisafirisha, kusambaza na kuuza zaidi ya kilo 100 za dawa hatari na za kulevya, zikiwemo heroini na fentanyl, kwenye Kisiwa cha Long, na hivyo kuchangia kwa makusudi janga la opioid ambalo limeharibu jamii zetu na kuchukua maisha ya watu wengi,” Brookyn US. Wakili Breon Peace alisema katika taarifa yake.
Rapa Fetty Wap mwenye umri wa miaka 30, ambaye alipoteza jicho kutokana na ugonjwa wa glaucoma alipokuwa mtoto, mara kadhaa amekuwa akipitia vipindi vigumu kwenye maisha. Mwaka mmoja uliopita alimpoteza kaka yake aliyefariki kwa kuuwawa, na baadae binti yake mwenye umri wa miaka 4 alifariki miezi michache iliyopita.
Awali alikamatwa mwaka 2019 kwa makosa matatu ya betri, na mwaka 2017 kwa malipo ya DUI baada ya polisi kusema alinaswa akiendesha gari kinyume cha taratibu za sheria, barabara kuu ya New York City.
Rapa huyo anafahamika zaidi kwa wimbo wake wa “Trap Queen,” uliofanikiwa kufanya vizuri sana mwaka 2014, ambao ulifika namba 2 kwenye chati za Billboard Hot 100.