Ni kwenye tamasha la #AstroWorldFest lililofanyika usiku wa kuamkia leo Novemba 6, 2021, huko Houston nchini Marekani, zimeripotiwa taarifa kuwa takribani watu 11 wamefariki Dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa vibaya kufuatia kukithiri kwa msongamano na vurugu zilizozuka wakati wa tamasha hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa mkuu wa kitengo cha Zima moto Sam Pena amesema kuwa tukio hilo limetokea punde tu, baada ya onesho kuanza, ambapo msongamano ulikuwa mkubwa huku kundi kubwa la watu likisukumana kuelekea lilipo jukwaa, kitendo kilicho sababisha vurugu zilizopelekea baadhi ya watu kukosa hewa ya kutosha kiasi cha kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa kutokana na kukanyagana.

AstroWorldFest licha ya kuwa ilipangwa ifanyike kwa muda wa siku mbili mfululizo Jumamos na Jumapili, lakini sasa limeahirishwa kufuatia tatizo hilo, mpaka sasa bado rapa Travis Scott hajazungumza chochote kufuatia kilicho tokea kwenye tamasha lake.

Takribani watu 84 wamepoteza maisha katika mlipuko Sierra Lione
Rais Mwinyi: ni jambo gumu nimepambana nalo